Friday, 22 November 2013

BABU SEYA MAISHA YAKE YOTE JELA: mahakama ya rufaa nchini tanzania imetupilia mbali ombi warufani wawili nguza viking na mwanaye, ambapo waliomba mahakama hiyo kufanya marejeo ya uamuzi wake wa awali wa kuwapata na hatia kama ambavyo hukumu dhidi yao ilivyo tolewa na mahakama ya hakimu mkazi kisutu tangu mwaka 2004. Nguza viking maarufu kama Babu seya, na watoto wake watatu walifungwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji na kuwalawiti watoto wadogo. Kesi hiyo imewashtua mashabiki wa viking, nchini tanzania na afrika mashariki. Mwana muziki huyo mwenye kuimba nyimbo za Rhumba, ambae ni mzaliwa wa DRC, ameishi Tanzania kwa miaka mingi na kuwa na mashabiki wengi. Walionekana kuwa watulivu wakati majaji walipo tupilia mbali ombi lao kutaka hukumu yao kubatilishwa.

No comments:

Post a Comment