Tuesday, 19 November 2013

20 WAUAWA NCHINI SOMALIA: watu ishirini wauawa nchini somalia katika shambulio la kujitoa muhanga katika kituo cha nchini somalia, Shambulio hilo limetokea katika mji wa Beledweyne karibu na mpaka nchini somalia. Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa gari lililo piga lango kuu la kituo cha polisi na kulipuka kabla ya watu wenye silaha kushambulia jengo hilo. Taarifa zinasema kuwa wengi wamefariki pamoja na maafisa wa polisi. Wapiganaji wa kiislamu wa Al-shabab wamekiri kuhusika na shambulio hilo. Maafisa wa polisi nchini somalia wamesema mlipuko huo umesababisha majeruhi kadhaa. Kamanda wa kundi la Al-shabab Mohammed Abu suleiman ameliambia shirika la AFP kuwa makomandoo wa Al-shabab ndio walio fanya shambulio hilo. Mwezi wa september kundi la Al-shabab lilisema kuwa lilifanya shambulizi la kigaidi katika kituo cha biashara westgate nchini kenya ambapo watu 67 waliuawa. Salumby7@live.com

No comments:

Post a Comment