Tuesday, 24 December 2013

DIAMOND AZINDUA VIDEO YAKE REMIX YA MY NUMBER ONE

Msanii wa muziki hapa tanzania nasib abdul ama diamond amezindia remix ya ngoma ya my number one kwa mara ya mwanzo mbele ya macho ya watoto waishio katika mazingira magumu dar es salaam.

Ngoma hiyo ambayo imegongwa nchini nigeria chini ya usimamizi wa kampuni ya nigeria na south africa kupitia producer clearence peter.

Mwana muziki huyo diamond ameigonga remix hiyo pamoja msanii mwengine kutoka nchini humo.

Tarehe 25 mwezi huu mchana diamond atakuwepo pale ukumbi wa leaders club mwanza.

Thursday, 19 December 2013

MSANII REDSAN AGONGA WIMBO MPYA NA ALIKIBA

Msanii redsan amegonga wimbo mpya na aliy kiba katika studio za homeboyz kenya.

Msanii huyo amegonga wimbo huo kupitia kwa produce wake sappy.
Producer sappy ameshare picha ya aliy kiba, redsan na sappy mwenyewe katika mtandao wa google ila
mimi sikuweza kuiweka hapa picha hiyo na samahani sana mpendwa msomaji.

Tuesday, 17 December 2013

MWANAMKE MJAMZITO INDIA APATA 'MISCARRIAGE' NA KUPOTEZA WATOTO KUMI.

Mwanamke mmoja raiya wa india aitwae anjua amejifungua mimba ili haribika njiani na kupoteza watoto kumi kwa kifo.

Kwa mujibu wa gazeti la indian express limesema kuwa mwanamke huyo alijifungua njiani wakati alipo kuwa akiwahi hospitalini nakujifungua njiani watoto tisa kisha mtoto mmoja wa mwisho kujifungua hospitalini.

Kwa mujibu wa madaktari wamesema kuwa mume wa mwanamke huyo alikuja hospitali akiwa na kitamba kilicho viringwa na ndani mkiwa na watoto tisa walio fariki.

Sunday, 15 December 2013

HAYATI NELSON MADIBA MANDELA AZIKWA

Raisi wa mwanzo na aliyekuwa shujaa wa afrika ya kusini hayati NELSON RIHLAHLA MADIBA MANDELA amezikwa jana kijijini kwao QUNU.

Maelfu ya wananchi na viongozi wa ngazi tofauti duniani wamehudhuria katika mazishi hayo.

Hayati nelson mandela alizaliwa mnamo mwaka 1918 huku kijijini kwao QUNU.
Raisi mandela alifungwa kwa takribani miaka 27.
Miaka 5 kati ya hiyo alifungwa katika gereza la posmo.
Na miaka miwili alifungwa katika gereza la paarl.
Na miaka iliyobakia 20 alifungwa katika kisiwa cha RUBBEN ISLAND akibanja mawe na kokoto.
Raisi mandela amewahi kuandila kitabu mashuhuri sana kiitwacho LONG WALK TO FREEDOM.

Saturday, 14 December 2013

MEL B KULA SIKU KUU IKULU KWA PAUL KAGAME

Mwana muziki wa new york Mel b mwaka huu anatarajia kula siku kuu ya christmas ikulu kwa raisi wa uganda PAUL KAGAME.

Amesema mwaka jana amekwenda kula na kufurahia siku kuu hiyo nchini Austraulia.

Mwaka huu ameupata mwaliko huo kupitia kwa watoto wawili wa bwana kagame jijini new york ama NY.

Monday, 9 December 2013

20% KURUDI KWA MAN WALTER

Msanii na mshindi wa tunzo tano za kilimanjaro mwaka 2011 "abass kinzasa" a.k.a "twenty parcent".

Amesema amependa kurudiana na producer wake huyo kwa ajili ya kuwaridhisha washabiki na jamii nzima.

Pia 20% amesema kuwa amesema ametaarisha ngoma yake mpya iitwayo "subira yavuta kheri" anatarajia kuitoa hivi karibuni.

Friday, 6 December 2013

MWILI WA NELSON MANDELA KUZIKWA HADI TAREHE 15 DECEMBER.

Raisi wa afrika ya kusini (SOUTH AFRIKA) jacob zuma ametangaza kuwa mwili wa hayati nelson rihilahlahla mandele utazikwa hapo tarehe 15 december katika kijiji cha qunu wilayani estern cape.

Thursday, 5 December 2013

New song: mumbi kutoka kenya ft fadhilee itulya

Mwana muziki kutoka kenya aitwad mumbi amepiga ngoma yake mpya iitwayo the end ikimshirikisha fadhilee itulya ndani yake download uone ubora wake tubidy.mobi

RAISI WA ZAMANI AFRIKA YA KUSINI (SOUTH AFICA ) AFARIKI DUNIA

Aliye kuwa raisi wa zamani na wa mwanzo afrika ya kusini nelson mandela amefariki dunia jana ya alkhamis tarehe 5 december 2013.

Nelson mandela amewahi kushinda tunzo ya nobel, na kutambulika sana afrika nzima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na raisi wa sasa nchi hiyo jacob zumma amesema raisi mstaafu mandelea alilazwa kwa kipindi cha miezi mitatu kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu.

Pia amesema nchi hiyo imepata majonzi makubwa mno kwa kuondokewa na mtu muhimu kama huyo.

Nelson mandela anakumbukwa kwa mambo tofauti likiwemo la kuondosha utumwa na kuleta uhuru nchini humo.

Pia kuondosha ubaguzi wa rangi.

Mungu amlaze mahali pema.raisi mandela amefariki akiwa na miaka 95.

Chanzo BONGO5/BBC NA CNN.

Tuesday, 3 December 2013

Ben pol kutaka kurudi dodoma kufanya research ya mziki wa asili

Msanii na mkali wa R&B hapa nchini tanzania ben pol amesema anataka kurudi dodoma ili kufanya research ya mziki wake wa asili.

Msanii huyo ameeleza kuwa anataka kwenda dodoma kwa ajili ya kufanya show kisha kubaki huko huko ili kutimiza research yake hiyo.

MPIRA UMEMALIZA KATIKA UWANJA WA FURAHA

Dakika 90 +4 zimemalizika katika uwanja wa furaha nchini kenya ambapo pambano kali lilipigwa kati ya kenya & zanzibar heroes.

Mpira huo umemaliza baada ya timu ya kenya kuichapa timu taifa ya zanzibar magoli mawili kwa sufuri 2-0 .

Magoli ya timu ya taifa ya kenya au harambe stars yalipachikwa wavuni mchezaji AIDO katika dakika ya 5 ya mchezo kupitia penanti baada ya beki wa zanzibar kumchezea madhambi mchezaji wa kenya.
Na goli la pili likipachikwa na ALLEN WANGA katika dakika ya 56 ya mchezo matokeo hayo yameifanya timu ya harambe stars kusonga hatua ya robo fainali huku zanzibar heroes na south sudan kurudi makwao.

Monday, 2 December 2013

MFALME WA RHUMBA CONGO AAGA DUNIA

aliekuwa gwiji wa rumba ''TABU LEY ROCHEREAU'' ameiaga dunia huko nchini ubelgiji. Mwana muziki huyo raiya wa DRC congo ambae ni mfalme wa tasnia ya rumba nchini humo, tabu ley ambae anasemekana kuzaliwa katika kipindi cha utawala wa wabelgiji mwaka 1937 au 1940. Mwana muziki huyo ambae alifariki akiwa na umri wa miaka 76 alifariki jumamosi huko ubelgiji. Tabu ley ambae alianza kuugua tangu mwaka 2008 kwa ugonjwa wa kiharusi.

ROSE NDAUKA

Msanii wa tasnia ya uigizaji nchini "ROSE NDAUKA" amesema kuwa anataka kujipa likizo ya kuacha kazi hiyo kwa kipindi cha mwaka mzima.

Ameyazungumza hayo msanii huyo katika gazeti la mwanaspoti nukuu ya kuwa "nataka kujipa likizo ya mwaka mmoja kwa sababu ya kuzongwa na kazi nyingi kwa mda huu ila nikimaliza nitaendelea na kazi hiyo".

Pia rose ndauka amesema anataka kutoka furaha kwa washabiki wake wa filamu pindi tu atakapo maliza kazi hizo